2
MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI. Dhambi zake zimemtenga na Mungu.Kwa hiyo hajui upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yake.

MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI

"Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu." (Warumi 3:23)

Mungu alimwumba mwanadamu kwa kusudi la kushirikiana naye, lakini mwanadamu alikwenda kinyume cha mpango wa Mungu. Alichagua kumwasi Mungu badala ya kumtii. Kumwasi Mungu ni kufanya dhambi. Mtu anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya dhambi.

MWANADAMU AMETENGANA NA MUNGU

"Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti" (Kutengana wa Kiroho na Mungu). (Warumi 6:23)

Mungu Mtakatifu - Mwanadamu Mwenye Dhambi

Picha hii ni mfana wa Mungu ni mtakatifu na mwanadamu mwenye dhambi. Kuna ufa mkumba kati ya Mjungu na Mwanadamu. Mwnadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa njia nyingi, dini, matendo mema, sala, n.k, lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi

Kanuni ya tatu inaeleza njia ya pekee ya kushirikiana na Mungu